Monday 31st March 2025, 21:49 pm

logo

The United Republic of Tanzania

CONTRACTORS REGISTRATION BOARD

  • crblogo

From The Press

photos are coming soon Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi CRB Mhandisi Joseph Nyamhanga, amezitaka Taasisi za Umma kuzingatia sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni zake za mwaka 2024 ambazo zinaelekeza kuwa mikataba ya miradi ambayo haizidi shilingi Bilion 50 inatakiwa itekelezwe na Makandarasi wazawa. Amesema hayo tarehe 20 Februari mwaka huu katika mwendelezo wa ziara ya Bodi ya Wakurungenzi na Menejimenti ya CRB inayofanywa katika mikoa minne ya Kanda ya kaskazini ambayo ni Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga kwa lengo la kukagua utendaji kazi wa Makandarasi na utekelezaji wa Miradi. "Sisi kama Bodi tunaendelea kushauri Taasisi za Umma ziendelee kuzingatia sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 pamoja na kanuni zake za mwaka 2024 kutoa kandarasi ndogo ambazo hazizidi shilingi bilioni 50 kwa Makandarasi wa ndani na hii itakua namna nzuri ya kuwajengea uwezo na kuhakikisha kwamba fedha hizi zinabaki hapa nchini”, alisema Mhandisi Nyamhanaga. Sambamba na hayo Mhandisi Joseph Nyamhanga, ametumia fursa hiyo kuzitaka kampuni za kigeni zinazojenga miradi nchini kutoa kandarasi ndogo (sub-contractors) zenye thamani kubwa ya fedha kwa Makandarasi wazawa ili miradi hiyo iwajengee uwezo. Mhandisi Nyamhanga aliyasema hayo wakati wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya CRB walipotembelea mradi wa usambazaji umeme vijijini (REA) katika mkoa wa Kilimanjaro wenye thamani ya shilingi bilioni 18.4 wenye urefu wa kilometa 270 unaotekelezwa na Mkandarasi Ceylex Engineering (PVT) Ltd kutoka SiriLanka. Akitoa taarifa kwa wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya CRB, Meneja wa mradi Mhandisi Sakina Mohammed amesema kuwa mradi huo wa usambazaji wa umeme vijijini (REA) ni wa miaka miwili na utasambazwa katika vitongozi 135 vya mkoa wa Kilimanjaro na mpaka sasa umefikia asilimia 11.6 ya utekelezaji wake. Katika hatua nyingine Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti ya CRB, walitembelea mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi wenye thamani ya shilingi trilioni 1.4 unaotekelezwa na Mkandarasi China Petroleum Pipeline Engineering Co. Ltd (CPP) katika kijiji cha Misino, Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga na kuridhishwa namna mradi huu unavyotekelezwa. Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya CRB Joseph Nyamhanga amempongeza Mkandarasi huyo kwa kuajiri watanzania kwa zaidi ya asilimia 70 pamoja na kutoa fursa ya kandarasi ndogo (Sub – Contractors) kwa Makandarasi wazawa, ambapo pia amewataka Makandarsi hao kukamilisha mradi kwa viwango na kwa wakati. “Ni jambo zuri kutoa ajira kwa wazawa, lakini pia nimefurahi ametoa kandarasi ndogo kwa Makandarasi watatu kwa kipande kinacho anzia mkoa wa Singida hadi hapa Tanga”. Amesema Nyamhanga. Akitoa taarifa ya mradi huo Willhel kiria ambaye ni meneja wa mazingira katika mradi huo,amesema mradi huo pia unazingatia uhifadhi wa mazingira kwani utekelezaji wake hauharibu miundombinu iliyopo. “Hapa katika kivuko cha barabara hii tunatoboa chini kwa urefu wa mita 48 ili tuweze kupitisha bomba, tukimaliza hapa tunahamia katika kivuko kingine”. amesema Kiria . Wajumbe hao wa Bodi pamoja na Menejimenti ya CRB, pia wametembelea kambi namba 16 ya Mkandarasi China Petroleum Pipeline Engineering (CPP) iliyopo katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga ambapo wameshuhudia maandalizi ya awali ya kambi ikiwa na utayari wa kuanza ulazaji wa bomba hilo la mafuta ghafi utakao anzia Kabaale - Hoima nchini Uganda na kuishia Chongoleani mkoani Tanga nchini Tanzania. Wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya CRB wanaendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika mikoa ya kanda ya kaskazini,ambapo wanatarajia kukamilisha Ziara yao jijini Tanga.
Photo by:Admin, 2025-03-26 05:54:08
photos are coming soon Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejiment ya CRB wameendelea na ziara yao tarehe 19 Februari mwaka huu ambapo wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa uwanja wa michezo jijini Arusha unaojengwa na serikali kwa thamani ya shilingi bilioni 286. Mwenyekiti wa Bodi ya CRB, Mhandisi Joseph Nyamhanga amemtaka Mkandarasi China Railway Construction Engineering Group Co. Ltd (CRCRG) kujumuisha Makandarasi wazawa katika ujenzi wa uwanja huo ili kuwajengea ujuzi na kuwa na uwezo. “Ni vizuri kuwatumia Makandarasi wa ndani kwa kazi zinazofuata katika mradi huu ili kuwajengea ujuzi ili uwanja huu utakapokamilika wawe na uwezo wa kukarabati wakati wa matumizi”, alisema Mhandisi Nyamhanga. Aidha mwakilishi wa Mkandarasi, Qs. Dennis Benito amesema kuwa wanafanya kazi usiku na mchana na hadi sasa wamefikia asilimia 25 ya utekelezaji na mpango wao ni kukamilisha mradi huo kabla ya muda wa mkataba ili watoe nafasi kwa wakaguzi wa michuano ya AFCON kukagua uwanja huo ili kutoa kibali cha fainali za AFCON 2027 yatakayofanyika katika uwanja huo. Katika hatua nyingie Wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya CRB walikagua mradi wa ujenzi wa jengo la matibabu ya moyo katika hosipitali ya rufaa ya kanda KCMC (Kilimanjaro Christian Medical Centre) wenye thamani ya shilingi bilioni 10 unaotekelezwa na mkandarasi Li Jun Development Construction Company Limited katika wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baada ya ukaguzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya CRB, Mhandisi Joseph Nyamhanga amemtaka mkandarasi kukamilisha mradi huo kwa wakati ili uanze kuwahudumia wananchi. Sambamba na hayo wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya CRB wamefurahishwa na mkandarasi huyo kujumuisha wazawa kama sub-contractors waliopewa kandarasi mbali mbali na kuwataka makandarasi hao kuhakikisha wanatekeleza mradi kwa viwango na kwa wakati. “Naomba nitoe wito kwa Makandarasi wa ndani walio kwenye mradi huu na Makandarasi wote wa ndani kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mikubwa hapa nchini ili kupata ujuzi na kujijengea uwezo wa makampuni yao ili waweze kutekeleza miradi mikubwa wenyewe," alisema Mhandisi Nyamhanga. Aidha Mkadiriaji Majenzi Salvatori Mbwelwa amesema kuwa mradi huo ni wa miaka miwili na umeanza tangu Julai mwaka jana na mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 30 ya utekelezaji wake. Pamoja na hayo Mhandisi David Mafuru kutoka hosipitali ya rufaa ya kanda KCMC ameshukuru ujio wa wajumbe wa bodi ya CRB katika mradi huo, na kueleza kuwa utaongeza kasi ya mkandarasi kukamilisha mradi huo kwa wakati ili kusogeza huduma ya matibabu ya moyo kwa wananchi wa kanda ya kaskazini ambao husafiri kwenda jijini Dar es Salaam kufata huduma hiyo. Aidha wajumbe wa Bodi hiyo wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la mahakama ya Afrika ya binadamu na watu katika eneo la Lakilaki Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wenye thamani ya shilingi bilioni 62 unaotekelezwa na mkandarasi CRJE (EAST AFRICA) LIMITED. Mradi mwingine uliotembelewa na Bodi hiyo ni pamoja na ujenzi wa jengo la taaluma katika chuo cha ushirika Moshi unaotekelezwa na Mkandarasi wa ndani TIL Constrctuction Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 3.2 na ujenzi wake umefikia asilimia 41.
Photo by:Admin, 2025-03-26 05:51:22
photos are coming soon Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi CRB Mhandisi Joseph Nyamhanga, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (REA) mkoa wa Manyara katika Wilaya ya Babati, Simanjiro na Kiteto, na kampuni ya China Railway Construction Electrification Bereau Group Company Limited (CRCEBG) kukamilisha mradi huo kwa wakati ili wananchi wapate huduma ya umeme. Amesema hayo tarehe 18 Februari mwaka huu katika ziara ya Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya CRB inayofanywa katika mikoa minne ya kanda ya kaskazini ambayo ni Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga kwa lengo la kukagua kazi za Makandarasi. Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa hatua ya serikali kusambaza umeme katika kila kitongoji nchini imelenga kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya umeme kwa gharama nafuu. Aidha msimamizi wa mradi Mhandisi Michael Masimbani amesema mradi huo umelenga kufikisha huduma ya nishati ya umeme katika kata 139 ambao thamani yake ni zaidi ya shilingi bilioni 21na miongoni mwa wanufaika ni pamoja na kitongoji cha Maisaka ambapo tayari nguzo zimeshasimikwa na nyaya zimeshavutwa na kwamba kilichosalia sasa ni ufungaji wa transfoma. Aidha ujumbe huo wa Bodi na Menejimenti CRB umetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa makumbusho ya Hifadhi ya Ngorongoro wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 23 unaotekelezwa na Mkandarasi China Railway 25 Group Ltd katika Wilaya ya Ngorongoro. Akitoa taarifa kwa wajumbe hao wa Bodi ya CRB Mjeolojia Ramadhan Khatibu kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro amesema makumbusho hayo yanatarajiwa kukamilika mwezi mei mwaka huu ambapo itaongeza idadi ya watalii watakao tembelea katika hifadhi hiyo. Sambamba na hayo Bodi hiyo imetembelea mradi wa upanuzi wa maji wa kilometa 48 unaotoka tenki la maji la Ngorbob jijini Arusha unaotekelezwa na Mkandarasi Jandu Pumblers Ltd katika eneo la Nanja wilaya ya Monduli ambao umelenga kutatua changamoto ya maji kwa wakazi wa wilaya hiyo na vijiji vya jirani. Pamoja na hayo Mwenyekiti wa Bodi ya CRB Mhandisi Nyamhanga amemtaka Mkandarasi Jandu Plumbers kuhakikisha anakamilisha mradi huo kwa kwa ubora unaotakiwa kwa kuzingatia gharama halisi kwa mujibu wa mikataba yao ili kutimiza azma ya Serikali ya kufikisha huduma ya maji kwa wananchi kwa wakati.
Photo by:Admin, 2025-03-26 05:48:21

Notice Board

Click "New" Icon Below To View Adverts

DELETED CONTRACTORS
QUALITY POLICY
KANUNI ZA UNUNUZI WA UMMA ZA MWAKA 2024
SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA YA MWAKA 2023
CONTRACTORS REVIEW INFORMATION FORM
ONLINE PROJECT REGISTRATION MANUAL
PROCEDURE FOR CHANGING NAMES, SHAREHOLDERS AND DIRECTORS

Video Adverts

Photo Gallery

Subscribes For Newsletter